Maswali Tanayoulizwa Sana (FAQ)



Swali: Je, kuna usajili wa akaunti kwenye 
LutanaFilms?
Jibu: Hakuna usajili wa akaunti yoyote wala shida nyingine yoyote unapotumia LutanaFilms.

Swali: Ni njia gani za malipo zinazotumika?
Jibu: Tuna njia kadhaa za kufanya malipo kwa kutumia simu za mkononi, soma hapa.

Swali: Nifanye nini wakati malipo yangu hayakufaulu?
Jibu: Tafadhali angalia kwanza kama una salio la kutosha katika akaunti yako ya malipo, kisha fanya malipo yako kama ilivyoelekezwa.

Swali: Je, ikiwa filamu iliyopakuliwa haiwezi kuchezwa?
Jibu: Kwa ubora wa filamu tulizonazo haitatokea kutocheza katika kifaa chako, jambo muhimu ni kwamba wakati wa kutazama filamu ni vema kutumia VLC media player ya hivi karibuni au media player nyingine ya hali ya juu.
  
Swali: Je, ikiwa filamu iliyopakuliwa haijatafsiriwa?
Jibu: Kumbuka kwamba filamu zote zilizopo kwenye tovuti yetu zimetafsiriwa kwa Kiswahili, ingawa tuna trela za filamu zilizotafsiriwa na ambazo hazijatafsiriwa kwa sababu ya sheria ya hakimiliki (“DMCA”) inayotuzuia kupakia baadhi ya trela zilizotafsiriwa kweye YouTube yetu.
  
Swali: Kwa nini siwezi kupakua filamu?
Jibu: Yawezekana unashindwa kupakua filamu kwa sababu ya kutokuwa na bando la kutosha, au kutokuwa na mtandao unaosapoti vema. Hivyo weka bando la kutosha na angalia mpangilio wako wa mtandao kama uko sawa, au tumia wi-fi.
 
Swali: Ninaweza kuzikuta wapi filamu zilizopakuliwa?
Jibu: Filamu ambazo umepakua kutoka LutanaFilms zitahifadhiwa ndani ya foda ya "Downloads" kwenye kifaa chako.
 
Tutafurahi kukuhudumia vema!